02 October, 2011

Mwakilishi wa kampuni ya PROFA ughaibuni  na ambaye ni mwanzilishi wa 
The Swahili Hub wa pili kulia naye alikuwepo kwenye DICOTA akiinadi kampuni mpya yenye kujihusisha na kufundisha lugha ya kiswahili nchini marekani pamoja na kuutangaza utamaduni wa Mtazania.
Kikubwa kilichojiri katika kongamano la dicota ni pamoja  na kuadhimisha siku ya uhuru wa nchi yetu Tanzania, ni hotuba ya mheshimiwa raisi Kikwete wakati akiwasihi watanzania waishio nje kukumbuka kuwekeza nyumbani.Alisema na mnukuu "hata kama ninyi hamuwezi kuwekeza,basi tafuta wawekezaji na muwalete wawekeze nyumbani"akimaanisha kwamba wote tuwe mabalozi wa nchi yetu Tanzania.

Pia katika tukio hilo,watanzania waliweza kuja kwa wingi na kukawepo na ubadilishanaji wa mawazo mbalimbali na kupeana taarifa mbali mbali kama vile,Wanajumuiya wa watanzania waishio Canada wameomba ushirikiano wa karibu na watanzania waishio Amerika ili na wao waandae kongamano kama hilo.

Pia mtanzania wa siku nyingi hapa America ambaye pia ni mchungaji katika kanisa la Bethel 
Dr.Nicku Kyungu Mordi naye aliwaalika watanzania kufika katika kongamano litakalofanyika November mwaka huu katika kanisa hilo lililopo mjini silver spring

No comments:

Search This Blog