30 October, 2010

Uchaguzi mpya na mambo mapya

Ni mategemeo ya wananchi walio wengi kwamba uchaguzi mpya utaleta mabadiliko mazuri na mengi katika nchi yetu iliyogubikwa na rushwa.Katika maswali niliyo wauliza Watanzania wengi waishio Washington DC,moja wapo lilikuwa kama ungekuwa unachaguliwa kuwa kiongozi wa nchi ya Tanzania ungetekeleza kitu gani kikiwa cha kwanza,asilimia sitini walisema watapambana na rushwa kwanza,na katika hili walisema wangewaadabisha wote waliohusika kwenye njama ya richmond,wizi wa mamilioni katika benki kuu,na wote wanaoshtumiwa kuhuza ardhi ya nchi yetu kinyemela.
Namimi halikahalika nakubaliana nao kwamba basi tutumie kura yetu kumpatia yule atakaye leta mabadiliko tunayoyahitaji na si wale wanaotaka kujinufaisha tu.

No comments:

Search This Blog