03 September, 2007

Wadau wote muliochangia


Kwanza napenda kumpongeza Michuzi kwa kuwezesha
watu kuwasiliana katika blog yake.Pili napenda kuwashukuruni wote mliochangia maana nimejisikia nyumbani kwani humohumo kuna watani wangu. Kuhusu makosa kidogo yaliyo jitokeza kwenye message, ni makosa ya kiufundi tu na wakulaumiwa si Michuzi aliyepost wala mimi niliyetuma na hata si ninyi mliochangia. Kwakifupi nilituma picha nne na kila picha ilikuwa na maelezo yake (..hii ni picha wakati wa spring hapa Marekani...)Sasa wakati wa ku-upload(kutuma) muda uliotumika pamoja na umbali vilisababisha kuleta speed iliyosababisha maneno yaliyo pandana na kusomeka isivyo dhamiliwa. Na hata picha kuonekana mbili tu. Najifunza kwamba siku nyingine sitatuma mambo mengi. Mlio ulizia kitabu, Kinapatikana hapa USA kwa order maalumu ila ukinipigia simu 301 768 7965 au ukaandika E-mail rwegap@yahoo.com naweza kukutumia sample kwa online. Hapa kinauzwa $10.tu Naomba usipige mahesabu kwa shilingi kwani kama unaishi Tanzania naweza kufanya mpango ukakipata kwa shilingi 2000/= iwapo nitaongea na Printers wa hapo Tanzania.

No comments:

Search This Blog