BLOOD PRESSURE
Mara nyingi wamama wengi wajawazito wamekuwa wakisumbuliwa na blood pressure ambayo inaweza kuhepukika kwani mara nyingi inachangiwa na kukosa amani,woga wa mama akiwa anakaribia kujifungua.
Blood pressure ikizidi mara nyingi mama mjamzito hushindwa kusukuma mtoto na ndipo madaktari ulazimika kumfanyia upasuaji jambo ambalo uongeza gharama katika kujifungua pamoja na kuongeza maumivu ambayo siyo ya lazima kwa mama.
MAZOEZI KWA MAMA MJAMZITO.
Mara nyingi wanaume wengine uwapa maraha ya kutosha wanawake wao jambo ambalo tunalihimiza hapa lakini wakati mwingine husahau kuwapa mazoezi wake zao wajawazito ikikumbukwa kwamba mazoezi kwa mama mjamzito ni muhimu kwaajili ya kubalance mwili ili uzito usiegemee upande mmoja tu. Wamama wajawazito wamekuwa wakikosa nguvu kwenye miguu kwa kadiri ya tumbo linavyozidi kuongezeka au uzito unavyoongezeka.Endapo mama ana mazoezi ya kutosha, basi misuri ya miguu usitahimili uzito wa tumbo na wengine wanaweza kwenda kazini mpaka siku ya kujifungua.
1 comment:
Jamani Faraja huyo..naona unadekezwa na huyo bwana wa kihaya hahahah.Mwaka huu wako dada
Post a Comment